Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Al Merrikh: Dakika 90 zitatoa majibu kwa Yanga

Osama Nabieh Kocha Mkuu wa Al Merrikh, Osama Nabih

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikijiandaa kwa mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Al Merrikh ya Sudan utakaopigwa katika Uwanja wa Chamazi siku ya Jumamosi Septemba 30.

Sasa katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Kocha wa Al Merrikh amezungumza kuelekea mchezo huo, ambapo amesema;

"Tupo kwenye wakati mgumu sana na tupo tayari kucheza tofauti na mchezo wetu wa kwanza tulivocheza

"Ukiachana na yote Yanga ni timu nzuri na ipo kwenye wakati bora sana lakini huu ni mpira lolote linaweza kutokea pengine hata yale ambayo hatujayatarajia kabisa"

"Mimi kama kocha sio jambo kubwa mabegani na wachezaji wangu wameshacheza michezo mikubwa dhidi ya Al ahly, Esperance , kwahiyo hainipi wakati mgumu sana"

"Dakika tisini zitatoa majibu ya maswali yenu yote na makosa yapo katika mpira kwahiyo tutajaribu kutumia makosa yote ambayo Yanga watayafanya.Sisi kama wachezaji kucheza nje ya uwanja wa nyumbani haijawahi kuwa tatizo kwetu"

"Yanga inazidi kuwa bora kila msimu kwahiyo tupo hapa kujitolea kwa dakika zote tisini ili tupate matokeo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: