Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kivuli cha Beno kinavyoitesa Simba, sasa watua Zalan FC

Majok Majok Majok Majok

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka katika klabu zimethibitisha kuwa Uongozi wa klabu ya Simba upo kwenye mpango wa kuinasa saini ya Mlinda lango wa klabu ya Zalan FC, Majok Majok (21).

Uongozi wa klabu ya Simba umeridhia kuanza Mchakato wa kuipata saini ya Mlinda lango huyo kwa haraka zaidi ili kuja Tanzania kuvaa viatu vya Mbrazil Luis Jefferson aliyeachwa kikosini kutokana na kutokidhi vigezo vya Mchezaji wa kigeni anayetakiwa kucheza ligi kuu Tanzania.

Kwa sasa itawalazimu Simba Sc kusajili mlinda lango huku wakilipa na faini kutokana na kusajili nje ya Muda wa dirisha la kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: