Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiungo wa Nabi apewa mkataba mgumu Yanga

Mudathir Yanga B Mudathir Yahya baada ya kuongeza kandarasi Yanga

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mkabaji wa Yanga, Mudathir Yahya ameboreshewa mkataba mpya wa miaka miwili wenye masharti mazito ya yeye kuondoka hapo.

Kiungo huyo ambaye ameungana na msafara wa wachezaji waliosafiri kwenda nchini DR Congo kwenda kucheza mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Mudathir alisajiliwa na Yanga katika dirisha dogo akiwa mchezaji huru ambaye alikuwa akiwaniwa Simba kabla ya kutua Jangwani.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, amemesema kuwa, kiungo huyo amepewa mkataba wenye sharti la kuongeza mwingine kama huo wa miaka miwili ukimalizika.

Bosi huyo alisema kuwa, kiungo huyo mara baada ya mkataba huo kumalizika atatakiwa kukutana na uongozi kwa ajili kufanya mazungumzo mapya ya kuongeza mkataba mwingine mpya.

Aliongeza kuwa Mudathir ameboreshewa mkataba mpya huo wa miaka miwili wenye thamani kubwa katika dau la usajili linalokafikia zaidi ya Sh 70Mil.

“Uongozi hautaki kufanya makosa kama yaliyojitokeza kwa Fei Toto, hivyo wameongeza umakini mkubwa katika mikataba yao mipya wanayowapa wachezaji wao.

“Lengo ni kuwadhibiti wasiondoke hapo kwa hapo kwa wale muhimu ambao wapo katika mipango yao ya muda mrefu kwa lengo la kuwa na timu bora na imara.

“Hivyo Mudathir mkataba wake huo aliopewa unamzuia kuondoka mara baada ya kumalizika hadi atakaposhindwana na uongozi ndio ataondoka,” alisema bosi huyo.

Akizungumza nasi, kuhusu sababu za kumuongezea mkataba kiungo huyo, Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji alisema: “Watu wengi wameonekana kuridhika na uwezo mkubwa ambao ameuonyesha Mudathir tangu ajiunge na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili.

“Lakini kiuhalisia kwa sisi tunaoufahamu vizuri uwezo wa Mudathir tunajua kuwa hajafikia hata asilimia 70 ya uwezo wake, hivyo hii ndiyo sababu kubwa ya kuamua kumuongezea mkataba ili apate nafasi ya muda mwingi zaidi kufikia kiwango chake bora na kuisaidia Yanga.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: