Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Yanga, Simba yamficha Kanoute

Robertinho Afurahia Ujio Wa Kanoute Kuwavaa Azam FC Sadio Kanoute

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Yanga, Uongozi wa kikosi cha Simba umeweka wazi kuwa kukosekana kwa kiungo wao wa kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute siyo kwa sababu ya majeraha yoyote bali ni kwa kuwa alipewa mapumziko maalum na atakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Yanga.

Kanoute hajaonekana kwenye michezo mitatu mfululizo ya Simba iliyopita ambayo ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ugenini na michezo miwili mfululizo dhidi ya Ihefu ule wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports na ule wa Ligi Kuu Bara.

Simba kesho Jumapili wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo ya mzunguko wa pili itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Yanga kumekuwa na maswali mengi juu ya wapi alipokuwa Kanoute na ikiwa alikuwa na majeraha, lakini habari njema ni kuwa Kanoute hakuwa na majeraha yoyote bali alikuwa na mapumziko maalum.

“Ni miongoni mwa wachezaji ambao wanaendelea na mazoezi na tunatarajia atakuwa sehemu ya mchezo huo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: