Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiraka ASEC Mimosas awaacha Simba kwenye mataa, ataibukia Jangwani?

Kiraka ASEC Mimosas Yao Kouassi Attohoula Sao

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za uhakika zinasema kuwa hapo awali Uongozi wa klabu ya Simba ulijaribu kufanya mazungumzo ya awali na Kiraka wa klabu ya ASEC Mimosas Yao Kouassi Attohoula Sao na mambo yalienda sawa sawia.

Wakati Uongozi wa Simba unajipanga kurejea tena Ivory Coast kwenda kuweka mambo sawa ya Kimkataba wakapewa taarifa kuwa tayari kiraka huyo anayemudu vyema kucheza nafasi zote za ulinzi (2,3 na 6) kuna klabu ameshamalizana nayo tena inatoka Tanzania.

Simba SC ikabidi warejee chini na kufanya maamuzi ya Kuachana nae. Uongozi wa Simba SC ulipanga kukamilisha usajili wa nyota huyo na baada ya kuona dili limevurugika wakaamua kufikia maamuzi ya kuwaobgezea kandarasi tena Israel Mwenda na Duchu kameta (aliyerejea).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: