Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipanya: Huyu Mayele anajua hadi anakera!

Mayele Na Mashabiki Yanga Mayele

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Singida United na Yanga, Kipanya Malapa ambaye wiki hii alikuwa gumzo baada ya kusambazwa kwa picha zake akiuza mishikaki kabla ya kuweka bayana hana mbambamba wala kujikweza, amemtaja straika wa Yanga, Fiston Mayele akidai anajua sana kucheka na nyavu.

Kipanya amesema licha ya nchi kushuhudia mastraika wa kigeni kuja kucheza nchini, lakini Mayele ni bonge la mchezaji ndio maana haishangazwi kwa misimu miwili mfululizo akiwa ndiye kinara wa mabao wa Yanga, huku akiwakimbiza wenzake katika Ligi Kuu Bara.

Kipanya amesema Mayele ni hatari, anajua kufunga na kupambana uwanjani, basi washambuliaji wengine wawe na wivu ili kula naye sahani moja.

Malapa alisema anashangazwa mastraika wengine wa timu hiyo wanavyokimbia kwenda kushangilia mabao ya Mayele na wakati wanashindwa kufunga wanapopata nafasi.

“Kushangilia bao ni jambo zuri la kuonyesha umoja lakini kuna wakati inabidi kama mshambuliaji uone wivu, kwa nini mwenzangu anafunga kila mara na mimi sifungi?

“Huwa nafuatilia mechi zinazochezwa ila kinachonishangaza ni washambuliaji ambao hawafungi halafu wenzao wakifunga ndio wa kwanza kwenda kushangilia ningekuwa mimi sifanyi hivyo,” alisema Malapa na kuongeza;

“Mfano Mayele akifunga unakuta kuna mwenye majukumu kama yake anakwenda kutetema bila wasiwasi na hajihoji kwanini hafungi kama mwenzake.

“Vitu kama hivyo nilikuwa sifanyi, kama sijafunga mechi tatu namwambia kocha asinipange tena ili nijiulize nakosea, lakini mastraika wa sasa wamekuwa kama mabeki, hii ni hatari kwa wazawa lazima wajiongeze kwa faida ya Stars.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: