Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Rivers: Yanga mbona wepesi tu!

Victor Sochima Kikosi cha Rivers

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Rivers United, Victor Sochima amewachimba mkwara washambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele na Kennedy Musonda kwa kuwaambia kuwa wanatakiwa kujua wanawajua vizuri ubora wao kutokana na kuifuatilia vyema Ligi ya Tanzania hivyo kazi yao kwake haitokuwa nyepesi kufanikiwa.

Sochima ametoa kauli hiyo ikiwa Yanga imepangwa kucheza na timu hiyo katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mchezo wa kwanza katika hatua hiyo unatarajia kupigwa Aprili 23, mwaka huu katika Uwanja wa Adokiye Amiesimaka uliopo katika Port Horcout, Rivers nchini Nigeria.

Akizungumza nasi, Sochima alisema kuwa wao kufika katika hatua hiyo imetokana na kazi kubwa waliofanya kwa kuweza kuwa mabingwa wa nchi hiyo hivyo wanawajua vizuri wapinzani wao ambao wanatakiwa kuwaheshimu tofauti wanavyowachukulia.

“Kwa sisi kuwa hapa, inaonyesha kazi ambayo tumeweka na ni jambo la kujivunia nchini Nigeria, sisi mabingwa wa ligi yetu na katika hatua ya hii ya mashindano tayari tunajua tutakutana na Yanga na kwa kuwa tunawafahamu vizuri basi tutakuwa tumejiandaa kuwatoa.

“Unajua tunafuatilia ligi yao kwa sababu tunafahamu, kuhusu Simba ambao ni wapinzani wao wa jadi lakini wanachotakiwa kujua haitokuwa rahisi kwa washambuliaji wao kupata nafasi ya kupata mabao kwetu maana hakuna ambacho hatujui kutoka kwao,” alisema Sochima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: