Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Rivers United amtaja Mayele, Musonda

Kipa Rivers Mlinda Lango wa Mabingwa wa Soka nchini Nigeria Rivers United, Victor Sochima

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Mlinda Lango wa Mabingwa wa Soka nchini Nigeria Rivers United, Victor Sochima amesema wanawafahamu vizuri Washambuliaji wa Young Africans Fiston Mayele na Kennedy Musonda, hivyo haitakuwa rahisi kuivuruga safu yao ulinzi.

Rivers United imepangwa kukutana na Young Africans katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku timu hizo zikitarajia kumalizana mwezi huu April kwa michezo ya nyumbani na ugenini.

Sochina amesema Young Africans wanatakiwa kufahamu kuwa, Rivers United sio timu ya kubeza na imedhamiria kufanya makubwa msimu huu, baada ya kushindwa kutinga Robo Fainali katika michuano ya Afrika msimu ulioopita.

Sochima amesema kuwa wao kufika katika hatua hiyo imetokana na kazi kubwa waliofanya kwa kuweza kuwa mabingwa wa nchi hiyo hivyo wanawajua vizuri wapinzani wao ambao wanatakiwa kuwaheshimu tofauti wanavyowachukulia.

“Kwa sisi kuwa hapa, inaonyesha kazi ambayo tumeweka na ni jambo la kujivunia nchini Nigeria, sisi mabingwa wa ligi yetu na katika hatua ya hii ya mashindano tayari tunajua tutakutana na Young Africans na kwa kuwa tunawafahamu vizuri basi tutakuwa tumejiandaa kuwatoa.”

“Unajua tunafuatilia ligi yao kwa sababu tunafahamu, kuhusu Simba ambao ni wapinzani wao wa jadi lakini wanachotakiwa kujua haitokuwa rahisi kwa washambuliaji wao kupata nafasi ya kupata mabao kwetu maana hakuna ambacho hatujui kutoka kwao,” amesema Sochima.

Mchezo wa Mkondo wa Kwanza kati ya Rivers United dhidi ya Young Africans inatarajiwa kupigwa Aprili 23, mwaka huu katika Uwanja wa Adokiye Amiesimaka uliopo katika Port Horcout, Rivers nchini Nigeria, huku mchezo wa pili ukipangwa kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam April 30.

Chanzo: Dar24
Related Articles: