Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda aitaka namba ya Tshabalala Simba

Zimbwe Mohamed Tshabalala Mtwara Mohammed Hussein 'Tshabalala'

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mohammed Hussein 'Tshabalala' ndiye mhimili wa Simba kwa eneo la beki wa kushoto wa timu hiyo na Taifa Stars, lakini sasa unaambiwa kuna dogo mmoja amejitokeza na kuitaka namba ya beki huyo mzoefu aliyewahi kuwika Kagera Sugar.

Kinda huyo anayekipiga Limbuka Akademy ya Kigamboni Dar es salaam, Valentino Amani, ndiye aliyeweka bayana kuitaka namba ya Tshabalala ndani ya Simba, licha tya kumtaja kama mchezaji anayemzimia na kupenda kuiga aina ya uchezaji wake.

Valentino alionyesha uwezo mkubwa kwenye mashindano ya vijana Wisdom Youth International Tournament 2023 yaliyomalizika hivi karibuni katika uwanja wa Fountain Gate Arena Jijini Dodoma na alipozungumza na Mwanaspoti, alisema bila woga kwamba yeye ndiye mrithi wa Tshabalala.

“Nampenda sana Tshabalala hadi jina langu la utani ni Tshabalala, naamini wakati wa kwenda kumrithi Simba umefika kwani ameitumikia kwa muda mrefu,” alisema kinda huyo mwenye miaka 17.

Kinda huyo alisema anaamini akisajiliwa Simba ana uwezo wa kuziba mashimo yote ya Tshabalala kwa uwezo alionao na jinsi anavyocheza kama beki huyo aliyeiotumikia Simba kwa misimu tisa mfululizo akitwaa nao mataji manne ya Ligi Kuu Bara na kufika nao robo fainali kadhaa za CAF.

Valentino anakiri soka la sasa limebadilika na vijana ndio wanatakiwa kupewa nafasi ya kucheza ili kuonesha uwezo wao.

“Najua bado sina uzoefu ila nitapambana kuhakikisha naaminiwa japo sio rahisi kama tunavyozungumza,” alisema kinda huyo kwa kujiamini.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: