Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachombeba Mudathir Yanga ni hiki

Mudathir Yahya.jpeg Kinachombeba Mudathir Yanga ni hiki

Sun, 3 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya amekuwa moto tangu ajiunge na timu hiyo dirisha dogo la usajili msimu uliopita akiwa kikosi cha kwanza, jambo lililowavutia wenzake kumzungumzia na kuona thamani yake inapanda.

Winga anayecheza kwa mkopo KMC akitokea Azam FC, Tepsi Evans alisema kulingana na aina ya mastaa waliopo Yanga na ushindani wa namba, anachokifanya Mudathir anaona kinastahili pongezi na kinampa heshima kama mzawa.

“Tangu msimu uliopita Mudathir alikuwa kwenye kiwango kizuri na msimu huu ni kama anaendeleza alipoishia, nikiwa kama mzawa siwezi kuacha kuthamini anachokifanya,” alisema.

Hoja yake iliungwa mkono na kipa wa timu hiyo, Wilbol Maseke aliyesema anaona mara nyingi Mudathir anahusika na mipira mingi muhimu na hatarishi kwa wapinzani, hivyo anaona anafanya kazi kubwa pengine kuliko kufunga.

“Simzungumzii kwa sababu nilikuwa naye Azam FC, ila uwezo wake ndio unafanya apate namba, kikubwa aendelee kupambana asijibweteke, naamini anaweza akajitengenezea ufalme wake,”alisema.

Mchezaji mwingine wa zamani wa timu hiyo na Simba, Amir Maftah alisema Mudathir ni mzawa anayejitengenezea heshima yake ndani ya Yanga na anamuona ataendelea kufanya makubwa, endapo tu akiendelea kumenteini kiwango chake.

“Alianza kuonyesha ubora wake tangu msimu uliopita, ila katika mechi mbili nilizomuangalia dhidi ya KMC na JKT Tanzania nimemuona anazidi kujiamini zaidi, jambo ambalo litamsaidia kucheza kwa kiwango kikubwa,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: