Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu kawa mtamu kuelekea 2023/24

Kibu Denis Wa Moto.jpeg Kibu Denis akifunga bao katika

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji Kibu Dennis aliyekamilisha msimu wa 2022/23 kwa kutupia mabao mawili na pasi mbili za mabao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ni kama amezaliwa upya, baada ya kumaliza kambi ya maandalizi mjini Ankara-Uturuki.

Katika mabao hayo mawili aliyofunga Kibu moja alimtungua Mlinda Lango Bora wa msimu wa 2022/23 Djigui Diarra akiwa nje ya 18 kwa shuti la mguu wa kulia.

Wakiwa kambini Uturuki nyota huyo alikuwa na zali la kucheka na nyavu kwenye mechi za kirafiki kama ambavyo alifanya mchezo dhidi ya Zira uliochezwa Julai 24 alipofunga bao dakika ya 33.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa, kila mchezaji ni kama amezaliwa upya kutokana na ubora wa kikosi chaope ambacho kiliwasili jijini Dar es salaam leo Jumatano (Agosti 02) majira ya Alfajiri.

“Wachezaji wote wa Simba ni kama wamezaliwa upya kwenye ubora kama ilivyo kwa Kibu Dennis ambaye alikuwa anapata nafasi za kufunga na kutengeneza mabao.

“Sijamzungumzia Fabrice Ngoma wala Clatous Chama na Luis Miquissone hapo unadhani nini kitatokea uwanjani? Mashabiki wa Simba ni muda wa kuendeleza furaha na kujitokeza kwa wingi kuwaona kwenye mechi zote.

“Katika tamasha la Simba Day itapendeza tukijitokeza kwa wingi ili kupata hizi burudani tukiwa wote kama ambavyo sera yetu inasema Simba nguvu moja,” amesema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: