Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu Denis apewe heshima yake

Kibu Denis, Usajili Kibu Denis apewe heshima yake

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, huu ni moja kati ya maneno ya hekima yaliyotumiwa na wahenga.

Sina haja ya kuelezea maana yake ila nachotaka kusema ni kwamba, mshambuliaji wa Simba, Kibu Dennis anapaswa kupewa haki yake yake.

Kibu ambaye alijiunga na Simba akitokea Mbeya City kwa haraka haraka ukiuliza mashabiki 10 wa Simba kuwa ni mchezaji gani wasiyompenda katika kikosi chao, watano kati yao watakutajia jina la Kibu.

Ila kwa wanaojua soka kamwe hawezi kumzungumzia vibaya mchezaji huyo, ndiyo maana hata kocha mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliviera amekuwa akimwanzisha katika kikosi chake cha kwanza.

Katika ushindi wa kishindo wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya na ulioishtua Afrika, Kibu alikuwa na mchango mkubwa.

Kutokana na hali hiyo basi mashabiki wa Simba wanapaswa kumpatia Kibu haki yake kama ambayo kocha wao anamwamini na kumwanzisha katika kikosi chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: