Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibadeni na matumaini kibao kwa Yanga

Kibadeni 1 King Kibadeni

Sat, 27 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema yupo tayari kuvaa jezi ya kijani na njano, ili kuipa sapoti Yanga, iweze kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger.

Akizungumza nasi, Mkongwe huyo amesema ana imani kubwa na Yanga kuanzia uongozi, benchi la ufundi na hata wachezaji hivyo anachowataka watumie faida ya kucheza nyumbani ili kushinda idadi kubwa ya mabao na kujiondoa kwenye presha watakapokwenda ugenini katika mechi ya marudiano.

“Mwaka 1993 nilikuwepo kwenye kikosi cha Simba kilichocheza Fainali na Stella Abidjan kifupi tulifanya makosa ya kushindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kuonesha kiwango bora kule Ivory Coast, sasa sipendi wenzetu Yanga warudie makossa hayo,” amesema Kibadeni.

Yanga itacheza na USM Alger Jumapili ikiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho, huku fainali ya pili ikipangwa kuchezwa Juni 3 huko nchini Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: