Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze apewa ofa mbili Yanga

Kaze Mali 1024x1024 Kaze apewa ofa mbili Yanga

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imerudi tena kwa kocha wao msaidizi, Mrundi, Cedric Kaze na kumpa ofa mbili, kati ya hizo achague moja itakayomrejesha na kumpa mkataba mwingine wa kuendelea na majuku yake.

Awali Yanga ilimpa ofa kocha huyo ambaye alizikataa baada ya kikao alichokaa na viongozi wa timu hiyo, kabla ya kwenda mapumzikoni Dubai.

Mrundi huyo ambaye amemaliza mkataba wake kikosini hapo, alitoa sharti la kuboreshewa maslahi yake ili asaini mkataba mpya, huku aking’angania apewe nafasi ya ukocha mkuu sambamba na kuongezewa mshahara mara mbili ya ule aliokuwa akilipwa mwanzoni.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, bado mazungumzo yanaendelea kati ya uongozi na kocha huyo, ndani ya wiki hii itajulikana hatma yake.

Mtoa taarifa huyo alisema uongozi huo umempa ofa mbili kocha huyo kati ya hizo achague moja ambazo ni kuwa kocha msaidizi au Mkurugenzi wa Ufundi.

“Wiki hii itajulikana hatma ya Kaze, kama ataendelea kufanya kazi na kocha mpya Gamondi (Miguel) ama hatoendelea kufanya kazi ndani ya Yanga.

“Kikubwa uongozi unataka kumalizana naye ili mara timu itakapoingia kambini kuanza Pre Seasson Jumatatu ijayo awepo sehemu ya timu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, hivi karibuni alizungumzia hilo la Kaze na kusema: “Hatma ya Kaze ndani ya Yanga ipo kwa kocha wetu mpya, kumbakisha au kumuondoa, hivyo tusubirie uamuzi wake.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: