Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Tumecheza na Rivers kwa hesabu kubwa

Kaze 10 Cedrick Kaze

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze raia wa Burundi amesema kuwa mpango namba moja wa timu hiyo katika mchezo wa jana dhidi ya Rivers United ya Nigeria ilikuwa ni kuhakikisha wanafuzu kwenda nusu fainali ya Kombe la Shirikisho badala ya kuwaza kufunga mabao.

Kaze amesema hayo wakati akihojiwa na Yanga TV mara tu baada ya mchezo huo war obo fainali ya Kombe la Shirikisho kumalizika katika Dimba la Mkapa.

“Ni furaha kubwa kwa wachezaji, wanachama, mashabiki na mpira wa Tanzania kuona kama kuna timu inaweza kufika nusu fainali. Kadri unavyosogea mbele ndipo unatamani kupata mafanikio zaidi, kwa sasa tuta concentrate na mechi zaijazo ili kuhakikisha tunapata tunachokitaka.

“Mechi za CAF sio rahisi, ukimfunguka mtu nyumbani kwake haimanishi ni dhaifu, Rivers ni timu nzuri na imeonyesha ushindani mkubwa kuanzia kwenye makundi.

“Kitu kikubwa ilikuwa ni kucheza na hesabu, mechi ya leo ilikuwa ni kufanikiwa kwenda nusu fainali, hivyo tulipaswa kucheza kwa nidhamu ili kupita na kujipanga na mechi zijazo.

“Tunaamini tuna kikosi bora, kilichokomaa na kinachoweza kutupa kile tunachokitaka, mechi ya leo ilikuwa na presha na historia yetu haikuwa nzuri, hivyo ni kitu kikubwa kufika nusu fainali, kila mtu amefanya kazi yake vizuri, amesema Kaze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: