Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Njooni muione Yanga ya tofauti

Kaze Mali 1024x1024 Kocha Kaze

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze raia wa Burundi amefunguka kuwa mashabiki na wanachama watarajie kuiona Yanga ya tofauti katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Us Monastir ya Tunisia.

Yanga kesho Jumapili watawakaribisha Monastir katika mchezo wa raundi ya tano ya hatua ya makundi ya Shirikisho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Mechi ya kwanza iliyopigwa Tunisia Yanga walilala kwa mabao 2-0.

Kaze amesema kuwa: “Sisi kama benchi la ufundi tumejipanga vizuri kukabiliana na mpinzani wetu Us Monastir siku ya Jumapili keshokutwa) na niwahakikishie tu wanachama na mashabiki wa klabu yetu kuwa programu zinaendelea vizuri na mtaiona Yanga ya tofauti sana katika mchezo wetu huo.

“Pia niwaombe sana mashabiki na wanachama wa klabu yetu ya Yanga waje uwanjani kwa wingi kuishabikia klabu yao ili tuweze kuondoka na alama tatu na kuendelea katika hatua zinazofuata za mashindano yetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: