Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaze: Atoboa siri alivyosuka mpango wa kuwatungua TP Mazembe

Fdgj Yanga Kaze Cedrick Kaze na wachezaji wake.

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha kutoka nchini Burundi Cedrick Kaze amesema haikuwa rahisi kuibanjua Tp Mazembe katika Uwanja wake wa nyumbani mjini Lubumbashi DR Congo, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya Makundi.

Young Africans ilicheza mchezo huo wa mwisho wa Kundi D, katika Uwanja wa Tp Mazembe na kuvunja mwiko kwa timu za Tanzania kushindwa kuondoka uwanjani hapo kwa kicheko kwa miaka yote.

Kocha Kaze ambaye alikabidhiwa jukumu la kuliongoza Benchi la Ufundi la Young Africans katika mchezo huo kufuatia Boss wake Nasreddine Nabi kurejea Ubelgiji kwa matatizo binafsi, amesema alipambana kadri alivyoweza kufanya kazi hiyo ipasavyo na kufanikiwa kwa asilimia 100.

Amesema nguvu ya Uongozi, Wachezaji na Ushirikiano alioupata kutoka kwa maafisa wengine wa Benchi la Ufundi, ilisaidia kupatikana kwa ushindi huo wa bao 1-0, lililofungwa na Kiungo Farid Mussa ambaye alichukua nafasi ya Mudathir Yahya Abbas katika kipindi cha pili.

“Haikuwa rahisi lakini ni mipango ambayo ilikuwepo kuanzia uongozi, benchi la ufundi na wachezaji ambao wamefanya kile walichoelekezwa na kufanikiwa kufikia lengo ambalo lilikuwa ni moja ya chachu ya kuona tunafika mbali.”

“Aina ya timu iliyopo Young Africans tunauona mwanga mkubwa kutokana na chachu ya ushindani wa wachezaji kwa wachezaji ambao pia wanatamani kuona wanaandika rekodi kubwa na kuacha historia ndani ya klabu hii.” Amesema Kaze

Ushindi huo umeiwezesha Young Africans kumaliza kinara wa Kundi D, ikiwa na alama 13 sawa na US Minastir ya Tunisia, huku AS Real Bamako ya Mali ikimaliza nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 05 na TP Mazembe inaburuza mkia ikiwa na alama 03.

Mbali na Young Africans timu nyingine zilizofuzu hatua ya Robo Fainali kwenye Shirikisho ni Asec Memosas, AS FAR. Marumo, Rivers United, USM Algiers na Pyramids.

Kati ya hizo Young Africans inaweza kupangwa na Pyramids (Misri), Rivers United (Nigeria) au USM ya Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: