Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya mwanasheria mpya wa Fei Toto

TFF FEI TOTO M Kauli ya mwanasheria mpya wa Fei Toto

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mwanasheria aliyemsimamia Bernard Morrison, Nduruma Majembe kushindwa na Yanga, Feisal / Wanaomsimamia wakaongeza nguvu wakamuajiri Mwanasheria Fatma Karume.

Baada ya Fatma Karume kushindwa na Yanga, leo Feisal / wanaomsimamia wamekuja na mwanasheria mwingine.

Jana Feisal aliambatana na mwanasheria aliyemsimamia Simon Msuva, Jasmin Razack katika ofisi za (TFF).

Walienda kuwasilisha ombi (TFF) kwa barua kulitaka shirikisho hilo kuuvunja Mkataba baina ya Feisal na klabu ya Yanga SC. "Waandishi msikurupuke kwenye kusema Feisal kaonewa ama ameshindwa, maneno mengi tuwe na uzalendo.

"Ninaomba tuvute subra, kwa mara ya kwanza leo Feisal kaleta ombi lake naimani kama litashughulikiwa. Nina imani na TFF, chombo pekee kinachoweza kuvunja Mkataba wa mchezaji ni (TFF)," amesema Jasmin Razack.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: