Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Mashabiki wa Yanga msipige mafataki kwa Mkapa

YANGA MASHABIKI ER.jpeg Kamwe: Mashabiki wa Yanga msipige mafataki kwa Mkapa

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imewataka mashabiki wake kuacha kupiga mafataki na tochi kwa wapinzani wao kwani wanaipa hasara klabu kwa kupigwa faini, kunyimwa baadhi ya vipaumbele kwenye mashindano hayo na kuonekana hawana nidhamu.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe wakati akizungumzia mchezo wao wa kesho Mei 10, 2023 wa Nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo gallants ya Afrika Kusini katika Dimba la Mkapa.

“Hii adhabu CAF wametupa kutokana na kuwasha moto sisi kwenye Mpira wa Afrika bado ni wanafunzi lakini kuna mamasta wa hayo mambo, mfano timu za Kaskazini na huoni kama wameadhibiwa.

“Nawaomba mashabiki wetu wasije tena na Fataki tukubaliane hatutofanya tena makosa. Ni kweli tumepokea Barua ya kutozwa faini dola 35,000 kwa makosa ya kuwasha fataki, Moshi na Tochi uwanjani pamoja na Basi la Rivers Utd kuvamiwa.

“Baadhi ya Matukio yanafanywa sana na Wenzetu waarabu lakini huoni wakidhibiwa hivyo Wananchi tunawaomba Waache hizi tabia kwa sababu tupo hatua nzuri ambayo inawezekana tunajaribiwa kutolewa kwenye ‘focus’ tunaomba Wananchi waache hizi tabia ili tusiwape sababu.

"Kadri unavyokuwa na nidhamu ndipo CAF wanakupa nafasi ya kuhodhi mchezo wa mwisho wa fainali, kwa hiyo wananchi watulie, waje na ngoma, waimbe wala wasipige mafataki na vitu vingine vilivyozuiliwa na CAF, tunautaka ubingwa,” Ally Kamwe, Afisa Habari wa Yanga Sc.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: