Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Kesho kuna bonge la 'sapraizi' kwa Mkapa

Ally Kamwe Afrika Kamwe: Kesho kuna bonge la 'sapraizi' kwa Mkapa.

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Yanga Sc, Ally Kamwe amewataka Wananchi kufika kwa Wingi Uwnaja wa Benjamin Mkapa Kesho kwani kuna ‘Sapraizi kubwa’ Yanga watafanya.

Kamwe amesema hayo leo wakati akihojiwa na WASAFI FM kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye Siku ya Mwananchi.

"Kesho tuna mambo makubwa matatu, la kwanza ni kuhakikisha mashabiki, wananchama wa Yanga na Watanzania wote watakaokuja Benjamin mkapa watakuja ku enjoy mchezo mzuri wa kaizer Chiefs na Ynaga.

"Uzuri wa Kaizer wamekuja kamili, wamesema hawajaja kutalii, wamekuja kuhakikisha wanapambana na Yanga kupima kikosi chao kwa ajili ya msimu unaokuja. Na sisi itakuwa sehemu sahihi ya kupima wachezaji wetu ambao tumewasajili kwa ajili ya msimu ujao.

"Kutakuwa na mechi ya viongozi wa Yanga na wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movies. Pia, kutakuwa na utambulisho maalum kwa wachezaji wetu tutakaokuwa nao msimu ujao.

"Watu wanauliza nani atatambulisha wachezaji hawa? Hii tuiache kama sapraizi, kesho wataalam waliokabidhiwa kazi hiyo. Mtu ambaye tutampa jukumu la kutambulisha hawa wachezaji ni mwamba kwelikweli, lazima awe fundi kuhakikisha wananchi wana burudika," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: