Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Kama mnataka kuibomoa Yanga, msajilini Eng. Hersi

Ali Kamwe Masimango Kamwe: Kama mnataka kuibomoa Yanga, msajilini Eng. Hersi

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema wale ambao wana mpango wa kuibomoa timu hiyo, basi wawapigie matajiri wao waje wamsajili Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, la sivyo Yanga hatobomoka.

Kamwe amesema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari kwenye hamasa kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS FC utakaopigwa Jumamosi ijayo katika Dimba la Chamazi.

“Kawaambieni Waarabu, kama kuna tajiri anataka kuibomoa Yanga SC, aje kumsajili Engineer Hersi,” amesema Ally Kamwe.

Ikumbukwe kuwa Yanga msimu uliopita walikuwa na straika wao aliyefanya vizuri kwa miaka miwili, Fiston Mayele raia wa Congo Dr ambaye kwa sasa amesajiliwa na Klabu ya Pyramids FC ya nchini Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: