Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamba ilikatika palepale kwenye ubovu

Bangala, Aucho N Mayele Mastaa wa Yanga

Sun, 2 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamba ngumu humpa nafasi mbebaji kusepa na mizigo anayohitaji kwa amani bila hofu lakini ikipata ubovu basi ni tatizo kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kukatika.

Kwenye Ligi Kuu Bara makosa yaliyofanywa na wachezaji baada ya kuunda Kamba ngumu itakayowapa pointi tatu ilipokatika walikwama kuunga ili kupata pointi tatu.

Hapa tunakuletea baadhi ya mechi ambazo zilikatika mara moja tu mzigo wa pointi tatu ukasepa mazima namna hii:-

YANGA 1-0 IHEFU Wakati Ihefu wakiamini wameukamata mchezo kutokana na mbinu ya kujilinda tangu mwanzo wa mchezo palepale pabovu kamba ilikatika wakatunguliwa bao moja mazima.

Dakika 45 za mwanzo Fikirini Bakari kipa wa Ihefu alikuwa imara hiyo ilikuwa Januari 17, mwaka huu, hakutunguliwa kipindi cha pili dakika 16 zilimtosha kulinda lango ila ile ya 17 akatunguliwa bao moja na Fiston Mayele ilikuwa dakika ya 62.

Uimara alioonyesha dakika 61 ulimeguka dakika ya 62 alipojichanganya kuutanguliza mpira mbele kisha Mayele akamzidi ujanja na pigo lake la kwanza liliokolewa na mabeki lakini lile la pili likazama nyavuni akitumia pasi ya Jesus Moloko.

Ruvu Shooting 0-1 Yanga Ruvu Shooting walidhamiria kuvuna angalau pointi moja mbele ya Yanga Uwanja wa Mkapa kwa kucheza mpira mkubwa ule wa mwendo wa mpapaso.

Dakika 32 kamba ilikuwa imara kwa pande zote ila ilipogota dakika ya 33 nahodha Mpoki Mwakinyuke katika harakati za kuokoa hatari ngoma ikazama nyavuni mazima.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire mara baada ya mchezo alisema kuwa waliwapa zawadi Yanga hasa kutokana na bao la kujifunga.

“Basi imetokea na Watanzania wameona namna wachezaji walivyopambana hilo bao sio la Yanga tumejifunga sisi hiyo tunaweza kusema ni zawadi kwao ila tumepoteza poiti tulizokuwa tunahitaji.” Ilikuwa ni Januari 23,2023.

Azam 1-0 Simba Mashabiki wa Simba walikutana na ubaridi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC walipotunguliwa bao moja na mtupiaji akiwa ni Prince Dube.

Azam FC hawakuwa na hiyana kwenye ubovu wa ulinzi katika kamba ya Simba wakapenya mazima na kumtungua Aishi Manula.

Mchezo pekee ambao Simba imepoteza pointi tatu mazima ilikuwa dakika ya 34 na hawakuwa na ubavu kuweka mzani sawa ilikuwa Oktoba 27, 2022.

YANGA 1-0 TANZANIA PRISONS Moja ya mchezo mkubwa kwa wachezaji wa timu zote mbili ulikuwa huu Uwanja wa Mkapa ambapo Prisons walikaza na Yanga nao walikaza mwanzo mwisho.

Ubovu wa kamba ulipatikana dakika ya 89 mtupiaji akiwa ni Feisal Salum ilikuwa ni Desemba 4, 2022 ngoma ikakatika jumlajumla kwa Wajelajela kuacha pointi tatu mazima.

PRISONS 0-1 SIMBA Wajelajela hawawakuwa na bahati walipokuwa Uwanja wa Sokoine kwenye mchezo dhidi ya Simba waliposhuhudia kamba ikikatika palepale walipojichanganya kwenye kuokoa hatari.

Ngoma ilipigwa mpaka dakika ya 84 kamba kotekote ilikuwa ngumu, dakika ya 85 pasi ya Kibu Dennis ikakutana na mwama Jonas Mkude akakata kabisa kamba na kuwaangusha Prisons ilikuwa ni Septemba 14, 2022.

Kagera Sugar 0-1 Yanga Haikuwa bahati kwa Kagera Sugar kuambulia hata pointi moja dhidi ya Yanga kwani penalti ambayo walipata walikosa na kuwapa pointi tatu mazima wapinzani wao.

Bao pakee la ushindi lilijazwa kimiani na Clement Mzize dakika ya 18 likadumu mpaka dakika ya 90 ilikuwa Novemba 12, 2022 Uwanja wa CCM Kirumba.

AZAM FC 0-1 IHEFU Oktoba 31, ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 1-0 Ihefu kwa bao la Prince Dube. Wana Ihefu wakasubiri kibao kigeuke mzunguko wa pili wakawachapa Azam FC bao moja tu.

Ilikuwa ni Machi 13, 2023 huku mtupiaji aliyekata kamba akiwa ni Rafael Daud, ‘Roth’.

SINGIDA BIG STARS 1-0 AZAM FC Uwanja wa Liti haukuwa salama kwa Azam FC walipotunguliwa bao moja na Singida Big Stars huku mkata kamba akiwa ni Bruno Gomez.

Pigo lake la faulo lilizama mazima kwenye nyavu na kuwafanya Azam FC kuyeyusha pointi tatu ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: