Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaizer Chiefs wamfungukia Skudu Makudubela 'Ni fundi'

Skudu Ews Skudu Makudubela.

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wamemwagia sifa kiungo mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela Skudu kuwa ni mchezaji mzuri na wanajivunia mchezaji kutoka taifa lao kuja kucheza soka la kulipwa Tanzania.

Skudo ambaye ni Mwafrika Kusini wa kwanza kucheza ligi ya Tanzania amejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Marumo gallants ya nchni humo kama mchezaji huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake na timu yake hiyo kushuka daraja.

Akimzungumzia Skudu, mshambuliaji Ranga Chivaviro ambaye wamecheza wote kwa pamoja Marumo, amesema;

"Nimefurahi kurudi tena Tanzania, mara ya mwisho nilikuja hapa nikiwa kama mchezaji wa Marumo Gallants, nilipata mapokezi mazuri sana, na leo tena nimerejea na Kaizer Chiefs ni jambo jema. Najua Watanzania wanapenda sana soka, sitegemi kingine zaidi ya kuonyesha soka bora kesho.

"Kwangu mimi itakuwa mara yangu ya kwanza kucheza mechi na Skudu Makudubela akiwa timu pinzani, ninafuraha kuhusu yeye najua amepokelewa vizuri hapa Tanzania kwa sababu Watanzania ni wakarimu," amesema Chivaviro.

Kwa upande wake, nahodha wa kaizer, Itumeleng Khune amesema; "Tunafurahi kuona Skudu akicheza hapa Tanzania, ligi yenu imekuwa kubwa na ina ushindani mkubwa, sio lazima tu tukacheze ulaya, hata hapa Afrika kuna timu nyingi kubwa ambazo mchezaji anaweza kuonyesha alicho nacho.

"Skudu ni mchezaji mzuri na ana kipaji, tunafurahi sisi kama Waafrika Kusini kutuwakilisha hapa Tanzania na tunamtakia kila la heri kwenye maisha yake ya soka," amesema Itumeleng Khune.

Skudu amewahi kucheza Timu mbalimbali zikiwemo Mamelod Sundowns, Orlando Pirates, Highland Park na Chippa United zote za Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: