Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC wakubali muziki wa Yanga "Tumejifunza"

Yanga Vs KMc 5 0.jpeg KMC wakubali muziki wa Yanga

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ofisa Habari KMC, Khalid Chukuchuku amekubali Yanga SC waliwazidi kiufundi ndio maana wamepata matokeo mazuri wameanza na ratiba ngumu sana ila ndio wanajipanga na kuchukua kama somo kwa Yanga ili kujiweka sawa kwenye mechi za mbele zaidi.

Chukuchuku amesema hayo jana mara baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga katika Dimba la Azam Complex Chamazi ambao ulimalizika kwa KMC kukubali kichapo cha bao 5-0.

“Yanga walistahili kushinda kwa namna ambavyo walicheza, wamecheza zaidi kwenye lango letu, wamemiliki mpira zaidi yetu na kutengeneza nafasi nyingi zaidi yetu. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya wao kushinda.

“Kwetu sisi kubwa tumeona mapungufu, labda ratiba ya hizi mechi ngumu za awali zinakupa nguvu ya kujifunza kuelekea michezo mingine ya ligi. Kwetu sisi tumelichukua kama somo na mwalimu Moulin atachukua hii kama homework kwake na wachezaji wake ili kurekebisha kwenye uwanja wa mazoezi.

“Hali ilikuwa mbaya dhidi yetu, mashabiki walikuwa wengi sana, presha kwa wachezaji ikawa changamoto lakini huu ni mwanzo, tumechukua somo hii kwa ajili ya maboresho tunaamini tutakuja vizuri mchezo ujao,” amesema Chukuchuku.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: