Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio aomba kazi Simba

Simba Vs Mwadui 20 Jamhuri Kihwelo ‘Julio’

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameutaka uongozi wa Simba kuwaamini wachezaji wao wa zamani akiwemo yeye ili kuipa timu hiyo maendeleo.

Julio alisema, kwa uwezo wake na nguvu aliyoitoa akiwa Simba, anastahili kuwa hata mshauri wa benchi la ufundi ili kuinyanyua timu hiyo.

Julio alisema: “Wenzetu Yanga, wanafanikiwa sana, mtu kama Said Maulid, mdogo wangu Mtwa (Mwanamtwa Kihwelo) wapo pale, timu kubwa ikiwa inacheza wanakwenda uwanjani na wanatoa mchango wao.

“Simba nipeni kazi hapo niwaoneshe, mimi nafanya kazi ya ushauri wa benchi la ufundi la Taifa Stars, mimi ni kocha wa timu za vijana, nitashindwaje kuwasaidia Simba?” alihoji Julio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: