Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio: Yanga walimchezea Feoi Toto kimkakati

MUDATHIRI FEI TOTO Julio: Yanga walimchezea Feoi Toto kimkakati

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Jamhuri Kihwelo Julio Alberto amesema kuwa Yanga SC walikuwa bora kila eneo kwenye mchezo wao dhidi ya Azam FC jana hivyo kusababisha wapinzani wao kushindwa kufurukuta na kujikuta wakiangushiwa kipigo cha bao 2-0 dakika za lala salama.

Julio amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii kwenye Dimba la Mkwakwani huku akiongeza kuwa Yanga walimchezea Fei Toto kimkakati ndiyo maana ubora wake ulikuwa hafifu uwanjani.

"Yanga walimudu sana eneo la kiungo na wakipata mpira wanapeleka mbele kwa haraka, kama mwalimu wa Azam angegundua hilo mapema angefanya kitu kizuri.

"Kingine Yanga wameboresha ambacho sijawahi kukiona wanaweza ku-press kwenye maeneo, hawakupi nafasi ya kucheza na wanakukaba muda wote, tactical discipline yao yao iko juu sana.

"Aucho kacheza vizuri, Mudathiri kacheza vizuri, ametembea na Fei Toto muda wote asipate nafasi ya kucheza, kwa hiyo Fei hakuweza kutoa pasi nzuri kama kawaida, hakupata nafasi ya kupiga shuti kwa hiyo utaona Yanga walimchezea kimkakati," amesema Julio.

Yanga sasa inasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Singoida Fountain Gate na Simba, ambaye atashinda watakutana kwenye fainali huku Azam akisubiri atakayeshindwa mchezo wa leo atakutana naye kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: