Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio: Viongozi Simba SC wasimpe Presha Kocha

Julio Jamhuri Jamhuri Kiwhelu "Julio"

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametoa angalizo kwa mabosi wa Simba kuwa wanapaswa kuwapa muda benchi la Ufundi kwanza.

Julio alisema usajili na kuonyesha uwezo uwanjani ni vitu viwili tofauti, hivyo ni lazima wanasimba wawe wavumilivu kwa sasa ili kuwapa muda mastaa wao wazoeane na wenzao kisha wawapime mbele ya safari.

“Niliitazama Simba katika mchezo wa Simba Day, na hata wa Singida, kuna matatizo madogo yanayorekebishika ila viongozi wawape muda wa kutosha benchi la timu hiyo na wachezaji katika kuweka mambo sawa” alisema Julio.

Julio alisema hata misimu minne mfululizo Simba ilivyokuwa haishishiki ndani na hata nje ilikuwa na kikosi bora ambacho kilikaa na kutengenezwa muda mrefu, hivyo wanasimba wasiharakishe mambo kwa sasa watawachanganya wachezaji na makocha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: