Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jezi za Simba kutambulishwa na majina ya viongozi wa Serikali

Jezi Simbaaas Jezi za Simba kutambulishwa na majina ya viongozi wa Serikali.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi ndivyo klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba Sc watazindua jezi zao mpya ambazo zitatumika kwenye msimu ujao wa 2023/24.

Taarifa zinaeleza kuwa kwenye jezi tano zitakazo zinduliwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro zitakuwa na majina ya viongozi wa Serikali mheshimiwa Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Rais wa Heshima wa Simba.

"Jezi zetu tano zitakazo zinduliwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro zitakuwa na majina ya viongozi wa Serikali mgongoni Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ally Mwinyi, Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson na Rais wa Heshima Mohamed Dweji Mo," amesema CEO wa Klabu ya Simba Sc Imani Kajula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: