Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Yanga lilotangulia Sauz kuweka mambo sawa

Yanga Adhabu CAF Jeshi la Yanga latangulia Sauz

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari mabosi wa Yanga kupitia kamati yao ya mashindano walitanguliza jeshi la watu sita nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuandaa mazingira rafiki ya kufikia na kufanya maandalizi timu hiyo kwenye mchezo wao wa mwisho.

Jumatano iliyopita Yanga, ilifanikiwa kucheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuwafunga mabao 2-0 Marumo Gallants ya Afrika Kusini katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga inahitaji sare, ushindi au kichapo kisichozidi bao 1-0 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Marumo utakaopigwa kesho Mei 17, mwaka huu huko Afrika Kusini.

Chanzo chetu kutoka Yanga kimesema kuwa, tayari uongozi ulituma watu wapatao sita kwa ajili ya kuandaa mazingira, ambapo wataongozana na CEO wao wa zamani, Senzo Mazingiza.

“Ukisikia kuwa hatupati matokeo kwa kubahatisha ni dhahiri uamini hilo kutokana na mipngo ya uongozi kuwa ya kibabe sana maana hapa tunapozungumza tayari kuna msafara wa viongozi sita wametangulia Sauz kuweka mazingira sawa.

“Kwa taarifa tu mipango yetu pia tunasaidiwa zaidi na baadhi ya wenyeji wa nchi hiyo ambao tuliwapata kupitia kwa CEO wetu wa zamani, Senzo na kwamba ataungana nao kutafuta kila mbinu za kuvuruga hujuma za Marumo,” kilisema chanzo hicho.

Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji timu hiyo kwa hatua waliofikia watatumia kila mbinu kuhakikisha wanatinga fainali na ikiwezekana kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: