Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Mkude amefanya makosa kuibusu nembo ya Yanga

Jemedari Mkude Jemedari Said: Mkude amefanya makosa kuibusu nembo ya Yanga

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kiungo mpya wa Yanga Jonas Gerald Mkude akiendelea kuliteka anga la michezo baada ya utambulisho wake wa kujiunga na Yanga jana Julai 12.

Mchambuzi wa michezo kutoka kituo cha EFM Jemedari Said amesema katika kitendo ambacho si cha kiungwana alichokifanya Mkude ni kuibusu nembo ya Yanga katika picha zinazosambaa akiwa ndani ya uzi wa Timu yake mpya.

Akizungumza Jemedari anasema;

"Jonas Mkude kubusu waziwazi nembo ya Yanga inaweza kuwa kosa kubwa sana anazi wa Msimbazi, kitendo hiki kinaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa kupendwa na kuheshimika kwa baadhi ya mashabiki wa Simba"

Je Mwanasimba Mkude amekosea au yuko sahihi, Mwananchi una lipi la kusema kwa kitendo cha nyota wenu mpya. Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: