Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jean Baleke: Kazi ya Kimataifa ndio kwanza tumeianza

Baleke Simba H.jpeg Jean Baleke

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji kutoka DR Congo anayeitumikia Simba SC ya Tanzania kwa mkopo akitokea TP Mazembe Jean Othos Baleke amefichua siri nzito ya kuendelea kupambana na kufanikiwa akiwa na kikosi hicho cha Msimbazi.

Baleke alifunga bao la kufutia machozi la Simba SC katika mchezo wa mwisho wa Kundi C dhidi ya Raja Casablanca iliyokua nyumbani mjini Casablanca Ijumaa (April Mosi) na kuchomoza na ushindi wa 3-1.

Mshambuliaji huyo ambaye kabla ya kutua Simba SC alikuwa akicheza klabu ya Nejmeh SC ya Lebanon kwa mkopo, amesema anaitazama Michuano hiyo ya Afrika kwa namna inavyoweza kuongeza maarifa zaidi kwake kama mchezaji mwenye mitazamo ya kufika mbali kwenye karia yake.

Baleke amesema kwenye michuano hiyo wanakutana na wachezaji wenye uwezo tofauti, hivyo kuna vitu vya kujifunza na kuvifanyia kazi katika majukumu yao ya kila siku, kuhakikisha wawapo uwanjani wanakuwa na vitu vipya vyenye manufaa kwa timu yao.

Amesema anaamini katika kujifunza maarifa mapya zinapotokea fursa kama za michuano ya CAF akiamini kazi yake inahitaji mbinu na ubunifu kila mara.

“Kwenye michuano ya CAF tunakutana na wachezaji wenye viwango tofauti, wanacheza ligi tofauti yapo ya kujifunza kwao, na wao yapo ya kujifunza kwetu, mchezaji anayeipenda kazi yake hachoki kupata vitu vipya kwenye kichwa chake.”

“Binafsi nimejifunza vingi kwanza kujiamini kunaongezeka, kutamani kufanya vitu vikubwa zaidi, mengine ni siri yangu yataonekana uwanjani wakati wa kuisaidia timu yangu kwenye michuano mbalimbali.”

Mshambuliaji huyo amefunga mabao matano kwenye Ligi Kuu alifunga dhidi ya Dodoma Jiji, Singida Big Stars na Hat Trick dhidi ya Mtibwa Sugar, kwa upande wa CAF ana mabao matatu.

“Kufunga ni jukumu langu kila ninapopata nafasi ya kufanya hivyo, maana yangu ni kwamba tunacheza watu wengi uwanjani nikiona mchezaji mwenzangu yupo nafasi ya kufunga natoa pasi, wote tunajenga Simba moja”

“Mbele yetu tuna kazi nyingi tunapaswa kuelekeza nguvu kupambana kwa pamoja ili tufanikiwe kwa pamoja, mfano baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya CAF tunapaswa kuongeza ushindani zaidi ili tufanikiwe.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: