Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Injinia Hersi atema cheche "Tunachukua yote"

Hersi Said Yanga Caamil Injinia Hersi

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuiongoza Yanga kufika hatua ya Robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la Shirikisho la Azam Sports, huku wakiwa karibu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, ametema cheche akibainisha kwamba, watapambana kuhakikisha wanashinda makombe katika mashindano yote wanayoshiriki.

Yanga Jumapili iliyopita walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir ya Tunisia na kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni mara ya kwanza kwao kufanya hivyo tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1935.

Kwenye mashindano ya ndani, Yanga tayari imefanikiwa kufuzu Robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports na inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kukusanya pointi 65 baada ya kucheza michezo 24, wakihitaji kushinda michezo mitatu ijayo kutetea ubingwa wao.

Akizungumza na Spoti Xtra, Injinia Hersi alisema: “Tumekuwa na mafanikio makubwa katika mashindano mbalimbali ambayo tunashiriki msimu huu, kwa maana ya Robo fainali ya Kombe la Shirikisho la ASFC na Kombe la Shirikisho Afrika.

“Lakini kwenye Ligi Kuu Bara pia tupo katika nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa wetu, kazi tuliyoifanya ni kubwa lakini tuna kazi kubwa zaidi ya kuhakikisha tunashinda makombe haya yote na tunaamini inawezekana.”

Kauli hiyo ya Injinia Hersi, ni wazi inawafanya wapinzani wao Simba kuwa na maswali ya kujiuliza kwani nao bado wanapambana kurejesha utawala wao wa kubeba Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), huku wenyewe wakifuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: