Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Injinia Hersi arudisha fomu urais Yanga

ENGINEER Hersi.png Injinia Hersi

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Enjinia Hersi Said amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa club ya Yanga SC katika Uchaguzi utakaofanyika July 10 2022.

Fomu za kugombea nafasi hiyo zimerejeshwa leo kwa Hersi kuwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela na Mzee Msumi ambao tayari wameweka wazi wanamuunga mkono Hersi Said katika Uchaguzi huo, Mwakalebela ameaga rasmi na kusema hatogombea nafasi yoyote Yanga.

“Kwa kifupi niseme kwamba dhamira Yanga haikuwa kuchukua fomu msimu huu na nimekuja hapa kwanza kuwaaga rasmi kwamba sitagombea na pili hatuwezi kuwaacha wana-Yanga kama watoto yatima ndio maana nimekuja kuunga mkono za Enjinia Hersi Said kugombea nafasi ya Urais Yanga SC,”Fredrick Mwakalebela

Nafasi za Uongozi zitakazogombaniwa Yanga ni nafasi saba ambazo ni Rais, Makamu pamoja na nafasi tano za wajumbe.

Chanzo: Tanzania
Related Articles: