Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Injinia Hersi: Hapa bado, Yanga bora zaidi inakuja

Hersi X Gamondi CRDB Injinia Hersi: Hapa bado, Yanga bora zaidi inakuja

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga SC Eng.Hersi Said amesema malengo ya klabu hiyo ni kujenga timu bora Zaidi kwa msimu ujao, ambapo watafanya usajili kulingana na mahitaji ili kukifanya kikosi hicho kufanya vizuri Zaidi kwenye mashindano mbali mbali.

“Tunaendelea kuijenga timu yetu. Tutafanya usajili mzuri kwa mahitaji ambayo yapo kwenye timu tuitoe timu hapa ilipo kuisogea mbali Zaidi. Hayo ndio malengo yetu kwa msimu ujao.” Amesema Hersi Saidi Rais wa Yanga SC

Hersi amesema hayo baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho Tanzania bara dhidi ya Azam FC jana usiku kwenye mchezo wa fainali uliochezwa visiwani Zanzibar. Kikosi hicho cha timu ya Wananchi kiliibuka na ushndi wa mikwaju ya penati 6 kwa 5, mchezo huu ulifika hatua ya penati baada ya mchezo huo kumalizika 0-0 ndani ya dakika 120.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: