Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ingia Clatous Chama, mlango uko wazi

Aziz Ki Chama Pacome Ingia Clatous Chama, mlango uko wazi

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kwa mbali ndege walisikika wakimtukuza Mwenyezi Mungu mwanga wa jua ulikuwa mlangoni mbele ya uso wa mgeni ambaye begi lake lilikuwa limejaa nguo nyingi sana.

Ile sauti ya boda boda ilisikika kwa mbali ikisema hiyo ndio ofisi ya injinia we bisha hodi tu.Uso wa mgeni ulipendezeshwa na tabasamu kabla ya kugonga mlango kwasababu ndoto ya kukutana na Aziz Ki ilikuwa imebaki sekunde chache kwa mkono kugusa kitasa cha mlango.Mgeni alivuta pumzi kisha neno hodi lilifuata sambamba na kitasa kutumika kama nyezo ya kuutembeza ule mlango.

Mlango ulifunguka kisha sauti iliyojaa hekima na upendo ilisikika ikisema mgeni karibu,kwa mbali paji la uso la mtu aliyeshika kalamu na karatasi lilionekana,kwa mujibu wa boda boda bila shaka huyu alikuwa Injinia aliyeamua kupanga matofali ya mpira wa miguu.

Ghafla baada ya Injinia kumuona mgeni alipaza sauti haaa haaa haaaa karibu sana sana sana Midfield Maestro hakika maombi yangu umeyatendea haki.Baada ya zoezi la mshangao Injinia alimuita Ali Never kisha akamwambia mpokee mgeni hilo begi hakikisha linakaa sehemu salama.

Injinia alifunga mlango akabaki na Mgeni wote walikaa kimya kisha makaratasi yakawa yanaongea kalamu ilikuwa inawapa somo kuhusu njia sahihi ya kupita,vifungu vya mkataba viligeuka Mc wa shughuli baada ya masaa kadhaa kupita Injinia alitabasamu kichwa kilisema ndio mikono ilisema Yes na mgeni alifurahi sana kwasababu ndoto ya kuitazama miguu ya Azizi Ki ilikuwa imekamilika juu ya meza ya Injinia.

Mgeni alishukuru sana kwa kupewa nafasi baada ya hapo akafungua mlango akatoka n’je kisha akampigia boda boda wake aitwae Chama aje kumchukua.

If truth shall kill them,let them die.

Ameandika Omar Kombo

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: