Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibrahim Bacca bado haamini macho yake

Fc Bacca Ibrahim Bacca bado haamini macho yake

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Kikosi cha Yanga, Ibrahim Bacca ametolea ufafanuzi kuwa hakuamini kuwekwa katika kikosi kitachoanza dhidi ya US Monastir kutokana na jinsi alivyoshtukizwa kabla ya siku mbili kuwa atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaoanza kucheza katika kikosi kitachoanza katika mechi hio.

Aidha ameeleza kuonyesha uthubutu wa kujituma hadi kupelekea kuwa fit na kuweza kuukabili mchezo huo wa ratiba za Michuano ya Shirikisho CAF ambapo timu yake YANGA iliibuka kwa ushindi wa Goli 2-0 US Monastir.

“Haikuwa rahisi siku mbili kabla ya mchezo kuambiwa mimi ni miongoni mwa wachezaji watakaoanza kwenye mchezo dhidi ya US Monastir, nilijiandaa kisaikolojia na kujiweka timamu kimwili ili kuweza kumwonyesha Kocha Nasriddine Nabi hajakosea kunipa nafasi” Ibrahim Abdallah ‘Bacca’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: