Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibrahim Bacca ‘Talisman’ mpya ya clean sheet za Nabi

Bacca X Nabi Ibrahim Bacca

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga wanatarajiwa kushuka uwanjani kuvaana na Marumo Gallants kutokea Afrika Kusini katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano hayo.

Mara baada ya mchezo huo Yanga watarudiana na Marumo katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa nchini Afrika Kusini, Mei 17, mwaka huu.

Yanga wataingia katika mchezo wa Jumatano wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kucheza michezo mitano kati ya saba iliyopita bila kuruhusu bao lolote ‘clean Sheet’ katika mashindano hayo, hasa baada ya kuanza kumtumia beki wao Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ ambaye amekuwa talisman ‘Karata ya bahati’ mpya ya Nabi kupata clean sheet kimataifa.

Championi Jumatatu, linakuletea mechi tano ambazo Bacca amehudumu kwenye safu ya ulinzi ya Yanga na kuifanya timu hiyo kumaliza dakika 450 bila kuruhusu bao lolote kama ifuatavyo;

YANGA 2-0 REAL BAMAKO Huu ulikuwa mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga walicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwa mabao ya Fiston Mayele na Jesus Moloko.

Katika mchezo huo safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa imara kiasi kwamba waliruhusu shuti moja pekee ambalo lililenga lango kati ya mashuti 11 ambayo yalipigwa na Real Bamako huku wenyeji pia wakimaliza mchezo kwa umiliki wa asilimia 53 dhidi ya 47.

YANGA 2-0 US MONASTIR Huu ni mchezo wa pili kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo, Bacca alianza kikosini katika mchezo ambao Yanga waliingia wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha mabao 2-0 ugenini nchini Tunisia.

Huu ni mchezo ambao Yanga walikuwa bora zaidi kati ya michezo yote ya hatua ya makundi ambapo walitawala mchezo kwa asilimia 60 dhidi ya 40 za US Monastir huku safu yao ya ulinzi chini ya Bacca ikiwa imara kwani waliruhusu shuti moja tu, kutoka kwa Waarabu ambalo pia halikulenga lango.

TP MAZEMBE 0-1 YANGA Yanga wakianza na mfumo wa walinzi watatu, huu ulikuwa mchezo wa kwanza Bacca kuanza kwenye kikosi Yanga wakiwa ugenini ambapo Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Huu ulikuwa mchezo mgumu zaidi kwa Yanga kwenye hatua ya makundi kwani licha ya ushindi walioupata Yanga waliruhusu mashambulizi mengi langoni mwao huku kipa wao Metacha Mnata akiokoa hatari saba ‘on target’ na kumfanya kutajwa kwenye timu ya wiki.

RIVERS UNITED 0-2 YANGA Mchezo wa kwanza wa hatua ya Robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao ulipigwa nchini Nigeria na kuwashuhudia Yanga wakipata ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Godswill.

Katika mchezo huu Bacca alianza tena kwenye mfumo wa walinzi watatu ambao ulitumika kwa dakik 45 kabla ya kubadilishwa kipindi cha pili na kocha Nabi kuiamuru timu yake kucheza 4-4-2.

Kwenye mchezo huo licha ya ubovu wa Rivers United kwenye safu yao ya ushambuliaji lakini ubora wa kuzuia wa Yanga uliwafanya wenyeji wapige mashuti 13 bila hata shuti moja kulenga lango.

YANGA 0-0 RIVERS UNITED Huu ni mchezo wa mwisho kabisa wa Yanga katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu hiyo rasmi ilifanikiwa kukata tiketi ya kucheza nusu fainali.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar Bacca alianza kwenye kikosi cha kwanza ambappo kwa mara nyingine tena aliisaidia Yanga kupata clean sheet nyingine huku Rivers wakishindwa kupiga shuti hata moja lililolenga lango kati ya mashuti manne ambayo waliyapiga.

Katika mchezo huo Yanga walitawala kwa asilimia 55 mchezo huo dhidi ya asilimia 45 za Rivers United.

Yanga 2- 0 Marumo Gallants Huu ni mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho uliopigwa Mei 10, 2023 katika Dimba la Mkapa na Yanga kufanikiwa kuondoka na ushindi mnono wa bao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants.

Bacca akisimama kwenye ukuta wa Yanga na kapteni Mwamnyeto, ameisaidia timu yake kwa mara nyingine kuondoka na clean sheet ya kibabe.

Bacca alitembea na straika wa Marumo, Ranga Chivaviro ambaye alishindwa kufurukuta hata pale alipopata nafasi, Bacca aliondoka na mali ama kumsumbua ili asipate utulivu wa kupiga.

Mechi hiyo muhimu kwa Yanga, bacca aliondoa hatari sita huku akipiga zaidi ya pasi 40 huku Wananchi wakimpigia upatu wa kuwa man of the match kutokana na kiwango bora alichokionyesha hasa kuwadhibiti washabmuliaji mahiri wa Marumo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: