Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibenge ndiyo mbadala sahihi wa Nabi - Mdau

Ibenge Na Mayele Ibenge ndiyo mbadala sahihi wa Nabi - Mdau

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiniambia Kocha gani anawafaa Yanga kuelekea katika nchi ya Ahadi basi nitakuambia Jina la Florent Ibenge.

Kocha anayelifahamu vyema soka la Afrika,akiwa na using ubingwa wa kombe la Shirikisho Afrika.

AS Vita, RS Berkane, Al Hilal na timu ya Taifa ya DR Congo kote huko amepita kwa mafanikio na amepata uzoefu mkubwa.

Asilimia kubwa ya Wachezaji wa Yanga kutoka DR CONGO wamepita katika mikono yake, Fiston Mayele,Yannick Bangala, Djuma Shabani, Jesus Moloko wote amewafundisha AS VITA bila kumsahau Tuisila Kisinda.

Hivyo hatakuwa na wakati mgumu Yanga kwa kuwa anawafahamu Wachezaji wengi wa Yanga anawafahamu pia wapinzani wa Yanga kama Simba, Azam na Namungo wote amewahi kukutana nao mara kadhaa.

Faida nyingine Ibenge ana ushawishi wa kuleta Wachezaji wakubwa,hivyo Yanga watafaidika na hilo. Shida ipo kwenye mshahara lakini ukitaka vizuri tumia pesa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: