Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu Bacca ni Ramos mtupu

Bacca Pic Huyu Bacca ni Ramos mtupu

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa Yanga Ibrahim Bacca ameweka rekodi ya kucheza michezo sita ya Kombe la Shirikisho Afrika bila ya kuruhusu bao tangu aingie katika kikosi cha Mtunisia, Nasreddine Nabi.

Bacca alijiunga na Yanga katika msimu uliopita akitokea KMKM ya Unguja, Zanzibar baada ya kuonekana katika Kombe la Mapinduzi na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nareddine Nabi.

Beki huyo akiwa na Yanga hakupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza katika msimu uliopita kabla ya kuaminika na kuanza kutumika katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Bacca alianza kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya US Monastir awa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika uliokuwa wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0, katika mchezo huo Bacca alicheza pamoja na Bakari Mwamnyeto, Dickson Job wakicheza mabeki watatu wa kati. Michezo mingine mitano aliyocheza dhidi ya Yanga 2-0 Bamako, Mazembe 0-1 Yanga, Rivers 0-2 Yanga, Yanga 0–0 Rivers na huu wa Nusu Fainali Yanga 2-0 Marumo Gallants.

Na michezo ambayo beki huyo hakucheza ni Monastir 2-0 Yanga, Yanga 3-1 TP Mazembe na Real Bamako 1-1 Yanga.

Ubora na kiwango hicho ambacho amekionyesha kimemfanya kuanza vizuri ndani ya timu hiyo, baada ya kuaminika na benchi la ufundi na kupewa nafasi ya kucheza katika michuano ya kimataifa.

Beki huyo jana alitangazwa kuingia katika kikosi bora cha Caf cha wiki hii ambayo michezo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika imechezwa wao wakicheza dhidi ya Marumo Gallants.

Wachezaji wengine saba wa Yanga waliingia katika kikosi hicho ambao ni Dickson Job, Diarra, Mudathiri Yahya, Stephane Aziz Ki, Bernard Morrison na Fiston Mayele.

Akizungumzia hilo Bacca alisema kuwa: “Kwangu ninajisikia furaha kupata nafasi ya kuaminika na kuingia katika kikosi cha kwanza, bado nina safari kubwa na mengi ya kuifanyia Yanga, niwaombe sapoti mashabiki sitawaamngusha.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: