Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu ni wakati sahihi kwa Chama kwenda Yanga

Chama Vs Jwaneng.jpeg Huu ni wakati sahihi kwa Chama kwenda Yanga

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji Clatous Chota Chama Msimu wa 2018/19 Simba SC ilikamilisha uhamisho/ usajili wa Clatous Chota Chama akitokea Lusaka Dynamos ya Zambia.

Misimu mitatu ya mafanikio akiwa na Simba ikawavutia Berkane, kama ambavyo mpira ni biashara 2021/22 Mwamba akajiunga na Berkane kutafuta changamoto mpya 2022 Mwamba akarudi tena Simba , kurudi kwake Simba hakukuwa bora sana kama awali kwa maana ya kushinda mataji hatimae msimu wa 2023/24 wamemaliza Simba ipo nafasi ya tatu NBC PL.

Chama hakuna experience mpya anayohitaji akiwa Simba, miaka 33 sasa anahitaji zaidi pesa na sio sifa na kwa maana hiyo huu ni muda /wakati sahihi wa yeye kuondoka Simba na ni wakataki sahihi pia Simba kuachana na Chama .

Tetesi zinasema kwa 51+ % Mwamba atajiunga na Yanga msimu ujao Kwa makusudi kabisa Simba wanatakiwa kuruhusu hili litokee kweli ili kujipa nafasi ya kutengeneza Simba mpya , slide ya 3 ni wachezaji waliofanya makubwa Simba lakini wakaondoka wakaiacha.

Uki-swipe slide ya pili utaiona Yanga ya 2020/21 , Yanga ambayo star alikuwa Mukoko Tomombe & Niyonzima lakini kwa ajili ya kujenga Yanga bora ,kutoka kwenye hiyo line up hapo amebaki Kibwana na Mauya pekee ambao nao hawana 100% ya kuanza kwa Yanga ya sasa.

Simba wasihofu juu ya tetesi pendwa ya kila msimu ambayo inaenda kuwa kweli kuelekea msimu ujao kama alivyoondoka Kagere , Lwanga na Mugalu basi waingine sokoni kutafuta bidhaa mpya na waruhusu Chama atafute changamoto mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: