Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huna haja ya kuilaumu Simba kwa mabao mawili ya Mtibwa

Matheo Anthony Lll Matheo alifunga mabao mawili dhidi ya Simba mchezo wa kwanza wa Ligi

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbele ya ukuta uliocheza mechi 49 bila kufungwa Abdul Suleiman Sopu alipiga hat-trick akiwa na Coastal Union.

Mbele ya mlinda mlango bora wa msimu, Sopu aliweka chuma mbili akiwa na Azam Fc. Pamoja na hayo yote haikuwazuia Yanga kushinda Ubingwa wa NBC na FA

Maana yake nini...?

Sopu hakufunga mbele ya walinzi dhaifu, Sopu hakumfunga Diarra mbovu, Bali Sopu alifunga mbele ya walinzi bora waliokuwa na siku mbaya kazini. Vivyo hivyo Matheo Anthony amefunga mbele ya ukuta bora uliokuwa na siku mbaya kazini

Nitakuambia kwanini...!

Unadhani Matheo Anthony ni bora kuliko washambuliaji wote wa Singida Fountain Gate? Au Matheo Anthony ni bora kuliko washambuliaji wote wa Yanga...? Mbona washambuliaji wa Yanga na Singida Fountain Gate hawakufunga bao mbele ya beki mbovu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: