Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hili ndilo jeshi kamili la Simba SC 2023/24

Simba SC Squad 2023 24.jpeg Hili ndilo jeshi kamili la Simba SC 2023/24

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Simba SC leo Agosti 6 imetambulisha kikosi chake kamili pamoja na benchi zima la ufundi kuelekea msimu mpya 2023/24.

Simba wametambulisha Kikosi kazi hicho katika kilele cha Tamasha la "Simba Day" lililofanyika katika Uwanja wa Mkapa Jijini Da er Salaam.

Tamasha hilo limehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alekuwa mgeni rasmi.

Simba inahitimisha Shughuli hiyo kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Timu ya Power Dynamos kutoka nchini Zambia.

Simba wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanazima ufalme wa Yanga ambao ndani ya misimu miwili wamelitawala soka la Tanzania kwa kubeba Ubingwa wa Ligi mara mbili mfululizo, Kombe la FA mara mbili mfululizo huku wakipigwa mara mbili katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Je watafanikiwa kuma;liza ufalme wa Yanga? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: