Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio kazi maalum ya Fabrice Ngoma Simba SC

Fabrice Ngoma Raja Casablanca Fabrice Ngoma

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fabrice Ngoma anakuja Simba akiwa ndio mtu ambaye ataweza kuokota mipira kutoka kwa walinzi wa kati na kuiamua kasi ya michezo kutokea dimba la chini kwa pasi fupi na ndefu. Hichi ni kitu ambacho si Kanoute wala Mzamiru aliweza kukifanya.

Ngoma pia anakuja kuongeza vitu viwili ambavyo Sadio Kanoute na Mzamiru Yassini walikuwa wanavifanya kila mmoja zaidi kwa kujitegemea.

Wakiwa karibu na lango na kutakiwa kuuathiri mchezo wakiwa hapo, Kanoute kajipambanua kama mtu anaeweza zaidi kufunga (rejea goli zake 2 dhidi ya Horoya, bao la kufutia machozi dhidi ya Azam nusu fainali ya ASFC na bao pekee dhidi ya Coastal Union kwenye mashindano hayo mwezi January) huku Mzamiru akijipambanua kama mtu anaeweza zaidi kupiga pasi za mwisho (rejea pasi zake 5 za mwisho kwenye NBC premier league msimu uliopita)

Ngoma amekuja akiwa na sifa ya kufanya vyote viwili kwa idadi ambayo inawiana kwani anaweza pia kutumika nyuma ya mshambuliaji inapobidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: