Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa ratiba ya mechi nne za Simba zinazofuata

Mgunda Simba Gd Hii hapa ratiba ya mechi nne za Simba zinazofuata

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ushindi wa kihistoria wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya Ac na kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, baadhi ya wachezaji wamekwenda kutekeleza majukumu ya timu za Taifa.

Nyota saba wa Simba wamejumuishwa katika vikosi vya timu za Taifa ambazo mwishoni mwa wiki watashuka dimbani kusaka tiketi za kufuzu michuano ya Afcon 2023.

Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yassin, Hennock Inonga, Clatous Chama, Peter Banda na Saido Ntibazonkiza wameruhusiwa kujiunga na timu za Taifa.

Wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wamepewa mapumziko ya siku chache kabla ya kurejea mazoezini kujiandaa na ratiba ya mechi zinazofuata.

Machi 31 Simba itakuwa ugenini Morocco kukamilisha ratiba ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa kwa mchezo dhidi ya Raja Casablanca.

Mechi mbili dhidi ya Ihefu Fc zitafuata. Wataanza na mchezo wa kombe la FA ambao utapigwa kati ya April 03/06 na baadae kusafiri mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa dimba la Ihefu, Aprili 08.

Baada ya mchezo huu Simba itarejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa April 16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: