Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa CV ya mshambuliaji mpya Yanga, Mayele akasubiri

Hafiz Konkoni Cv Mshambuliaji wa Yanga, Hafiz Konkoni

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Julai 29 Yanga walimtambulisha Mshambuliaji mpya Hafiz Konkoni kutoka Klabu ya Bechem United inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ghana.

Tanzaniaweb tunakuletea wasifu (CV) ya Mshambuliaji huyo ili upate kumfahamu na pengine utoe mawazo yako kuona je anaweza kuwa mrithi sahihi wa Fiston Mayele.

Kwa experience Konkoni anaonekana kuwa na uzoefu mkubwa kuliko Mayele kwani amecheza mpka nje ya Afrika na amecheza Timu za Taifa Ghana kwa ngazi zote.

Jina: Hafiz Konkoni Urefu: 1,85 m (futi 6.1in)

Hafiz alizaliwa Nchini Ghana, Amecheza kwenye timu za taifa za vijana Ghana zote kuanzia

U-17

U-20

Senior Team (Ghana)

Hafiz konkoni amekulia kwenye Academy ya Chelsea Barekum ya hapo Ghana kisha akasajiliwa na klabu ya Bechem United kwenye timu za vijana na 2018 Alipandishwa timu ya wakubwa.

ELIMU BINAFSI: Ni muhitimu kwenye chuo cha Ghana kiitwacho TUMU (College of education. Ni public college).

MSIMU WA 18/19 - Klab ya Bechem United ilimuuza kwenda Ulaya katika klabu ya Merit AYSK ya Nchini Cyprus kisha klabu hiyo ikamtoa kwa mkopo kwenda Baf Ulku Yudu ya hapo hapo Cyprus,

30 June 2019 - akarejea Merit baada ya mkopo kumalizika, akapata injury iliyomuweka nje kwa muda mrefu. 14 November 2019 akarejea kuamua kurejea zake Bechem United,

Msimu wa 2021/22 alikuwa akiuguza majeraha alicheza mechi chache. Ameitumikia timu hiyo kwa misimu (3).

TAKWIMU ZAKE ZA UFUNGAJI (Muda wote akiwa Bechem United)

Michezo 97

Magoli overall 46

Magoli ligi kuu 34

22-23 Ligi kuu ya Ghana (MAFANIKIO YAKE)

Michezo - 26

Mfungaji namba mbili -15

Nafasi ya timu kwenye ligi -3

Assists alizotoa -3

Mafanikio aliyotwaa kwa msimu wa 22/23

Kikosi bora cha Mwaka cha ligi kuu

Mshindi wa pili kwenye mbio za MVP

18 June 2023, Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Chris Hughton alimuita Hafiz Konkoni kwenye timu ya taifa, Ghana dhidi ya Madagascar AFCON Qualifies.

Yanga kwa sasa ni miongoni mwa Vilabu vikubwa Afrika kwani ina ubavu wa kupambana na vilabu

Yanga wameshinda kuwania saini yake dhidi ya timu mbalimbali kama zifuatazo ;

Vs Hearts of OAK (Ghana)

Vs Al Hilal (Sudan)

Vs Asante Kotoko (Ghana)

Vs Future FC (Misri)

Vs ASEC Mimosas (Ivory Coast)

Vs Al Ahli Tripoli (Libya)

Sio jambo rahisi kuitwa Timu ya Taifa ya Ghana.

Kuna Mataifa ndani ya Afrika yamewekeza vipangi sana kwenye soka.la Vijana tena kwenye Nchi mbali mbali kunwa Kama Ufaransa, Uholanzi, Ubelgiji na Hata Hispani,

Huu sio Usajili bora tu bali Usajili Mkubwa Afrika kutokana na Takwimu zake akiwa ligi kuu ya ndani, Amekuwa mshambuliaji mwenye Uwezo kufunga magoli kwa msimu 10+.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: