Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hicho chombo kilichosaini Simba mtatafutana

Yahaya Mbegu To Simba Hicho chombo kilichosaini Simba mtatafutana

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Deal done! Ndiyo utakavyoweza kusema kwa beki kushoto wa Ihefu FC ya Mbalari, Mbeya, Yahya Mbegu ambaye usajili wake umekamilika Simba huku akisubiria utambulisho pekee.

Simba imefanikiwa kuipata saini ya beki huyo, baada ya kushinda vita kubwa iliyokuwepo kati yao na Singida Fountain Gate ambayo inakwenda kucheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Beki huyo ni kati ya wachezaji waliokuwa katika mipango ya muda mrefu na Simba katika kuwasajili ambaye amemaliza mkataba wa kuichezea Ihefu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi, beki huyo tayari amewaaga viongozi na wachezaji wenzake kwa kuwaambia hatokuwa sehemu ya kikosi hicho katika msimu ujao.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uongozi umetakia heri beki huyo huko atapokwenda kuanza maisha mapya akiwa na kikosi cha Simba katika msimu ujao.

Aliongeza kuwa beki huyo wakati wowote atatambulishwa mara baada ya dirisha la usajili kutangazwa kufunguliwa, licha ya taratibu zote kukamilika za usajili.

“Mbegu tayari ameshakamilisha taratibu zote za usajili Smba ikiwemo kupiga picha akiwa anasaini mkataba Simba, kilichobakia ni kutambulishwa pekee.

“Simba wamefanikiwa kuipata saini ya Mbegu ni baada ya vita kubwa ya usajili kati yao na Singida Fountain Gate ambayo nayo ilimpa ofa nzuri ambayo yeye hajaikubali.

“Simba walimpa nzuri, kingine mchezaji mwenyewe alikuwa anakwenda katika timu kubwa ili akapate ushindani mkubwa wa kucheza,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kuwa: “Wapo wachezaji wengi tuliofanya mazungumzo na kufikia muafaka mzuri wa kuwasajili, hivyo ni suala la muda kuwatangaza.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: