Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hersi aanza kushusha majembe Yanga

Khanyisa Mayo Khanyisa Mayo

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imeanza mazungumzo ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Cape Town city ya South Africa, Khanyisa Mayo mwenye umri wa miaka (24).

Mshambuliaji huyo ni kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya South Africa msimu huu akiwa na mabao (12) sawa na Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns.

Anauwezo wa kucheza winga pia.

Rais wa Yanga amesema; "Tutamsajili mshambuliaji mmoja kutoka hapa Nchini Afrika kusini msimu huu, ni mapema kumtaja, lakini niwaahidi tu kuwa ni mshambuliaji hatari anayefanya vizuri kwa sasa," amesema Eng. Hersi Said ambaye ni Rais wa Yanga.

Jioni hii, Mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohamed (GSM) amewasili Nchini South Africa kuungana na timu yake.

Mpaka sasa viongozi wote wakuu wa Yanga wamewasili Nchini Afrika kusini kama ifuatavyo. Imethibitishwa.

☑️ Ghalib Said Mohamed (GSM)

☑️ Eng. Hersi Said - Rais

☑️ Arafat Haji - Makamu

☑️ Andre Mtine - CEO

Wajumbe wa kamati tendaji

☑️ Munir Said

☑️ Alexander Ngai

☑️ Yanga Makaga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: