Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize awapa neno wachezaji wa Yanga

Yanga Mwed Ngao Harmonize awapa neno wachezaji wa Yanga

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Fleva na shabiki kindakindaki wa Klabu ya Yanga, Harmonize ameshindwa kuficha hisia zake na kufunguka kuhusu maumivu ya timu yake kufungwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa Jadi, Simba SC jana.

Harmonize ambaye ni CEO wa Konde Gand amesema kuwa wao kama mashabiki wa Yanga wamewasamehe wachezaji wote na wapo tayari kuendelea kuwaonga mkono ili wafanye vizuri zaidi katika michezo ya ligi na michuano mingine kurejesha furaha ya Wananchi.

Yanga jana ilikubali kupoteza mchezo huo kwa kufungwa peanti 3-1 baada dakika 90 kumalizika kuhu timu zote zikitoka sare ya bila kufungana katika dimba la CCM mkwakwani Tanga.

"Dear Yanga Sc players this is how I fill now, najua kila Mwananchi wa kweli anajisikia hivi. Tumewasamehe na niwahakikishie tupo pamoja kwenye hiki kipindi kigumu.

"Lets them talk, wacha watuchambe kwa sababu kwao ni ndoto yao. Tumepokea kama bahati mbaya na tupo tayari kwaajili ya Ligi Kuu Tanzania, tunawaamini na mnatembea na furaha zetu tunataka ligi kuu kwa mara ya 3," amesema Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: