Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakika kizuri hakidumu!

Mayele Helmy S Hakika kizuri hakidumu!

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku zote vizuri hua havidumu, hii imedhihirisha kwa watu muhimu ndani ya Klabu ya Yanga, Kocha Nasreddine Nabi, Fiston Mayele, Feisal Salum na Prof. Helmy Guel.

Mayele ameondoka ana magori takribani 50+ tangu aitumikie klabu, mfungaji Bora msimu2022/23, MVP wa ligi kuu na top scorer kombe la shirikisho Afrika.

Feisal Salum alie tuonesha ubora wa nini namba10 anatakiwa kufanya kutoa mchango mkubwa kwa klabu alisaidia klabu kufuzu fainali za kombe la Azam dhidi ya Simba msimu wa 2021/22.

Helmy alikua ni kocha waviungo mwenye elimu ya juu ya fitness coach, ametoa mchango mkubwa kwa wachezaji, fitness ya wachezaji ilimalika sana, majeruhi kwa wachezaji hayakuonekana mara kwa mara.

Nabi yeye ameondoka kama shujaa wa msimu, sub zake ziliwaangamiza wapinzani wake na kuipaisha Yanga. Hata timu ikifungwa kipindi cha kwanza, Nabi alijua namna ya kumaliza mchezo kipindi cha pili.

Hakuaminiwa mwanzoni wakati anakuja Tanzania, walisema kimataifa anapigwa, ni kocha wa ndani tu, lakini alichokifanya Kimataifa, kitabaki kuwa alama isiyofutika katika mioyo ya Wananchi.

Ubingwa makombe yote ya ndani misimu miwili mfululizo, fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza, acha aitwe Profesa wa mpira.

Hakika vizuri havidumu, Yanga watawamiss na kuwakumbuka kwa Mchango wenu Daima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: