Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara amlipua Fei Toto "Kupanga ni kuchagua"

Manara Fei Toto Haji Manara na Fei Toto

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Klabu ya Yanga ambaye amefungiwa na TFF, Haji Manara amemchana mchezaji wa timu hiyo, feisal Salum 'Fei Toto' kuwa anatakiwa kufanya maamuzi na kurejea dimbani la sivyo kipaji chake kitapotea.

Manara amesema hayo kufuatia michezo miwili ya Taifa Stars ambayo Fei Toto alicheza lakini hakuonyesha kiwango kizuri kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu bila kucheza.

Fei Toto ana mgogoro na timu yake ambapo ameshawasilisha maombi TFF akiomba kuvunja mkataba wake na Yanga.

"Jana na last week kule Misri nilikutazama vizuri, kila hatua na kila moment, nilikuona una ubora ule ule ila unachokosa ni ile speed yako ya maamuzi.

"Na hii imesababishwa na kukosa kwako match fitness, mcheza mpira hata a-train vipi kama hapati mechi za kucheza kuna kitu kitapungua tu kwake.

"Ndiyo maana timu nyingi zinakuwa na mechi maalum kwa wale wachezaji wasio na nafasi sana katika vikosi vyao, au wale waliotoka katika majeruhi.

"Fei narudia tena na tena na tena, haya ni maisha yako wewe, hakuna mbadala na hakuna mwema zaidi yako wewe binafsi, na hayupo mbaya katika maisha yako kuliko wewe mwenyewe.

"Kupanga ni kuchagua mdogo wangu, turudi kula Ugali na Sugar au nije kesho unipeleke na mimi nikale Urojo Foro?

"Mechi zinakuhitaji ili ubaki bora, wenzio wote wamerudi katika timu zao, wewe upo mtaani, usikubali hivi vitu, football ni ajira yako na maisha yako dogo. Au ile transaction ya leo imekuchanganya mwana?," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: